Mwinyi atuma ujumbe mzito Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Dec 2017
Mwinyi atuma ujumbe mzito Yanga
Baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Chalenji, mlinzi wa kushoto wa Yanga Haji Mwinyi ameutahadharisha uongozi wa Yanga kuwa atalazimika kuondoka kama hatapata nafasi ya kucheza.

Mwinyi amenukuliwa na mtandao wa GOAL, akisema kwamba hatakuwa na uvumilivu tena iwapo kocha George Lwandamina hatampanga.

"Natambua kuwa hatuwezi kucheza wachezaji 12, uwanjani lakini kitendo cha kukaa benchi mfululizo kwangu hakinifurahishi kwani nahofia kupoteza kiwango changu nivyema kama sitokuwepo kwenye mipango ya timu basi wanaruhusu kuondoka nikatafute sehemu ambayo nitapewa nafasi ya kucheza," amesema Mwinyi.

Aidha Mwinyi amesema ataendelea kucheza kwa kujituma ili kumshawishi kocha Mzambia George Lwandamina, kumrudisha kwenye kikosi cha kwanza vinginevyo anapanga kuachana na timu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Hakuna shaka juu ya kiwango cha Haji Mwinyi sasa, michuano ya Chalenji imemuimarisha zaidi.

Lakini bado linabaki kuwa jukumu la kocha kuamua ni nani acheze kwa kuangalia mahitaji ya timu kwa wakati huo.

Yanga inakabiliwa na michuano mingi sana mwaka 2018 hivyo hapana shaka Mwinyi atapata nafasi ya kucheza muhimu ni kuwa mvumilivu tu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’