Yanga kesho Jumanne itashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Gwambina Fc ukiwa ni mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom
Kuelekea mchezo huo Yanga itaendelea kukosa huduma ya baadhi ya wachezaji ambao ni majeruhi/wagonjwa
Kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' ameongezeka katika orodha ya wachezaji majeruhi akiungana na Yassin Mustafa na Mapinduzi Balama ambaye anaendelea kuimarika
Aidha beki nahodha Lamine Moro, alipata majeraha mazoezini na imeelezwa kuwa hali yake inaendelea vizuri
ADVERTISE HERE