Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kushika kasi ambapo kesho Jumanne vinara wa ligi hiyo Yanga watashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Gwambina Fc
Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ambao ulipigwa Misungwi, Mwanza ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Huu ni mchezo wa pili msimu huu lakini wakati huu Yanga ikiwa nyumbani
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo uliopita, Yanga imepania kuendeleza wimbi la ushindi ili kuhakikisha hawapotezi matumaini ya kuwania ubingwa
Jana watani zao Simba walipata ushindi wa bao 1-0 kule Shinyanga dhidi ya Mwadui Fc na sasa wamesogea nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 52
Ushindani umekuwa mkubwa katika nafasi tatu za juu kwani hata Azam Fc nao wamekuwa na mwenendo mzuri katika michezo ya karibuni wakishika nafasi ya tatu na alama zao 50
Huu ni mchezo mwingine ambao Yanga inahitaji alama zote tatu
Mchezo utapigwa kuanzia saa moja usiku