Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amesisitiza kuwa bado hawajakata tamaa na mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu kwani hakuna jambo lisilowezekana
Jana Yanga ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ys Biashara United na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 54
"Bado tunaongoza ligi, sasa hivi wakisema ligi imesimama sisi tutakuwa wa kwanza. Nia yetu iko palepale, kikubwa ni kushinda kila mechi ambayo iko mbele yetu ili tuweze kufikia malengo yetu. Mimi naamini kwenye mpira kila kitu kinawezekana, sisi tunaendelea kumuomba mungu ili tuweze kufikia malengo yetu," amesema Niyonzima
"Jambo jema kwetu sasa tunatengeneza nafasi nyingi. Ni bora kutengeneza nafasi halafu tukashindwa kuzitumia. Sasa hivi tunatengeneza nafasi baadae tutajiuliza kwa kiasi gani tunazitumia nafasi hizo"
Niyonzima alikuwa sehemu ya kikosi kilichopata ushindi dhidi ya Biashara United jana ingawa yeye aliingia katika kipindi cha pili
Keshokutwa Jumanne Yanga itashuka tena uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Gwambina Fc