Highlights, Yanga ilivyoichapa Biashara United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2021
Highlights, Yanga ilivyoichapa Biashara United

Yanga jana imepata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Ulikuwa mchezo ambao Yanga ilihitaji ushindi huu ili kuinua morali ya wachezaji wake baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha

Katika mchezo huo Yanga ilionyesha dhamira ya kusaka matokeo tangu dakika ya kwanza huku Biashara United wakicheza kwa kujilinda zaidi

Kuanzishwa kwa Carlos Carlinhos eneo la kiungo kuliinufaisha sana Yanga katika umiliki wa mpira na hata katika kuanzisha mashambulizi

Carlinhos alitawala kiungo, akishirikiana na Mukoko kuifanya timu iwe na uwiano mzuri wakati inashambulia na hata pale inapozuia

Safu ya ulinzi ilikuwa chini ya Abdallah Shaibu na Dickson Job. Pamoja na baadhi ya mashabiki kuonyesha wasiwasi pale orodha ya kikosi ilipotolewa na Job kuanza katika kikosi cha kwanza, bila shaka baada ya mchezo hawakuwa na la kusema zaidi ya kupongeza

Kwa hakika pacha ya Lamine Moro na Bakari Nondo Mwamnyeto katika eneo la ulinzi, iko hatarini kuvunjwa na vijana hawa

Yacouba Songne akafunga bao lake la sita akimalizia krosi murua iliyochongwa na Adeyum Saleh baada ya Mukoko, Kaseke, Carlinhos, Saido, kutengeneza mipango

Songne amefunga katika mchezo wa pili mfululizo kwani ndiye aliyefunga bao la Yanga katika mchezo uliopita dhidi ya KMC

Kwa ujumla jana Yanga ilicheza vizuri zaidi ukilinganisha na mechi zilizopita karibuni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’