Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga leo wamefufua matumaini kwenye mbio za ubingwa baada ya kuichapa Biashara United bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yacouba Songne ndiye aliyefunga bao pekee la Yanga kwenye dakika ya 58 akimalizia krosi murua ya Adeyum Saleh
Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi wakisaka bao la mapema lakini safu ya ulinzi ya Biashara United ikiongozwa na Abdulmajid Mangalu walikuwa imara
Kocha Juma Mwambusi alifanya mabadiliko katika kikosi kilichoanza ambao kwenye safu ya ulinzi aliwaanzisha Abdallah Shaibu 'Ninja' na Dickson Job wakati Carlinhos akianza badala ya Feisal Salum
Ninja ameendelea kufanya vizuri katika mchezo wa pili mfululizo wakati Job naye amedhihirisha kuwa ulikuwa uamuzi sahihi kwa Yanga kumsajili kutoka klabu ya Mtibwa Sugar dirisha dogo




Yanga ilihitaji ushindi leo, alama tatu muhimu zimepatikana
Wananchi wameendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 54