Shirikisheni wachezaji wa zamani katika usajili - Chambua

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Apr 2021
Shirikisheni wachezaji wa zamani katika usajili - Chambua

Kiungo wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua, amewataka viongozi wa timu hiyo kubadilisha mfumo wa usajili wa wachezaji wanaoutumia sasa kwa ajili ya kuhakikisha msimu ujao wanapata nyota wenye uwezo mkubwa wa kuitumikia klabu hiyo

Chambua aliyetamba na Yanga kuanzia katikati ya miaka ya 1980 hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990 amesema kwa kubadilisha mfumo wa usajili, klabu hiyo itaingia mikataba na wachezaji wenye tija na uwezo wa kuitumikia timu yao vizuri.

Nyota huyo alisema umefika wakati viongozi na wadhamini wakawatumia watu sahihi ikiwamo wachezaji wa zamani katika kufanikisha mchakato wa usajili na kuachana na njia wanayotumia hivi sasa.

"Viongozi wanatakiwa kufikiri sana kuwa nani anaweza kuwasaidia kupata wachezaji wazuri?. Fedha zipo, wafadhili wapo na wanaonyeshwa na nani wachezaji wazuri ili waende wakasajili? Sisi wachezaji wa zamani mbona tupo lakini hatutumiki? Mimi nipo kwenye Kamati ya Ufundi. Hii inaleta shida namna ambapo hata wachezaji kutoka nje wanavyokuja ni wachezaji, lakini kuna baadhi hawatoshi, hawana uwezo wa kuichezea timu kubwa kama ya Yanga," Chambua aliliambia gazeti la Nipashe

Nyota huyo ameungana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, ambaye alisema Yanga ina baadhi ya wachezaji ambao hawajitumi na wengine hawana uwezo na sifa ya kuichezea timu hiyo.

Muro ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga alishangazwa kuona timu hiyo kuwa na mastraika ambao wamekaa kipindi cha miezi mitano hadi mwaka bila kufunga bao hata moja na kuongeza Yanga ya sasa siyo kama anayoijua yeye ya 'Kampa Kampa Tena.'

Naye beki wa zamani wa klabu hiyo, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' alisema wachezaji wa timu hiyo ndiyo wanaowaangusha viongozi kwa kushindwa kupambana na kupata matokeo chanya.

Alisema anachokiona ni kila siku zinavyozidi kusonga mbele ndiyo viwango vya wachezaji wa Yanga vinaporomoka na kuiweka timu hiyo katika wakati mgumu kwenye mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Yanga yenye pointi 51 ndio vinara wa ligi hiyo ikicheza mechi 24 na katika msimamo inafuatiwa na mabingwa watetezi, Simba yenye pointi 49 lakini imeshuka dimbani mara 21

Jioni Yanga inashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Biashara United ukiwa ni mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’