Nahodha wa Yanga Lamine Moro amesema wataendelea kuipigania timu ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya msimu huu
Baada ya mfululizo wa matokeo ya sare, mashabiki wameanza kukata tamaa katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu
Hata hivyo Mghana huyo amesema kukata tamaa ni msamiati ambao haupo katika vichwa vyao wachezaji
Watahakikisha wanapambana mpaka dakika ya mwisho licha ya kukiri kuwa ushindani ni mkali
"Sisi hatujakata tamaa, kwa wanaodhani hivyo wanajidanganya. Kwa sababu wachezaji wote fikra zetu tumezielekeza katika kuwania ubingwa"
"Nimeona maoni ya watu wakikosa imani nasi lakini nawaambia tuko imara, hatuwezi kukata tamaa, tutapambana mpaka mwishoni mwa msimu"
"Kila mechi kwetu ni kama fainali, ushindani umekuwa mkali lakini nasi tunaongeza juhudi ili tufikie malengo yetu," alisema Lamine
Keshokutwa Jumamosi Yanga itashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Biashara United katika mchezo mwingine wa ligi kuu ambao Wananchi wanahitaji alama zote tatu
Kwani matokeo tofauti na ushindi ni wazi yatazidi kudidimiza matumaini hayo ya kushinda ubingwa