Mabadiliko ya makocha ni 'pasua kichwa' Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
15 Apr 2021
Mabadiliko ya makocha ni 'pasua kichwa' Yanga

Moja ya eneo ambalo viongozi wa Yanga hawawezi kukwepa lawama ni katika maamuzi ya kupata kocha mpya pale wanapofanya mabadiliko

Kwa kiasi kikubwa msimu huu Yanga imeathiriwa na mabadiliko ya makocha katika muda ambao sio sahihi

Tangu mwanzo mwa msimu Yanga ilichelewa kumleta kocha mpya. Baada ya mpango wa kumpata kocha Cedric Kaze kukwama, wakamuajiri Zlatko Krmpotic wiki moja kabla ya ligi kuanza

Baada ya siku 37 wakaachana na Krmpotic na kurudi kwa Kaze ambaye pia walilazimika kumsubiri kwa takribani wiki tatu kabla ya kuwasili nchini

Naye akatua wiki moja kabla ya ligi kurejea kutoka kwenye mapumziko ya kalenda ya Kimataifa mwezi Oktoba 2020

Hata hivyo Kaze akaondolewa baada ya miezi mitano tu licha ya kocha huyo 'kuipotezea' Yanga muda mrefu wa kumsubiri

Utaratibu ukawa uleule tena baada ya Kaze kuondolewa wengi walitarajia kocha mpya angewasili mapema hasa ikizingatiwa kulikuwa na mwezi mmoja wa mapumziko kutokana na kalenda ya Kimataifa

Lakini siku chache baada ya mchakato wa kusaka kocha mpya kuanza, uongozi ukatangaza wameamua kumuachia timu kocha Juma Mwambusi mpaka mwisho wa msimu ingawa kulikuwa na taarifa kuwa uongozi ulikusudia kumleta kocha mpya mapema ili apate nafasi ya kukifahamu kikosi kwa undani ili imsaidie katika maboresho mwishoni mwa msimu

Baada ya sare dhidi ya KMC presha ya kuleta kocha mpya imerejea tena na pengine kama Yanga haitapata matokeo Jumamosi katika mchezo dhidi ya Biashara United, mwishoni mwa wiki kunaweza kushuhudiwa mabadiliko mengine ya kocha

Kwa kweli hapa viongozi hawawezi kukwepa lawama za mashabiki kwani wamekuwa wazito sana kufanya maamuzi hasa katika kuajiri makocha wapya

Mara nyingi timu inapofukuza kocha lazima iwe tayari na mpango wa mbadala wa kocha huyo

Kocha wa muda hapaswi kuachiwa timu kwa muda mrefu kwani ikiwa hivyo, yakifanyika mabadiliko lazima yataathiri mwenendo wa timu

Mabadiliko ya kocha wakati huu hayawezi kuisaidia sana Yanga kwani kocha mpya hatakuwa na muda wa kuitengeneza timu yake vile anavyotaka

Ni vigumu kuandaa timu wakati kukiwa na presha kubwa ya matokeo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’