Yanga inaendelea na mchakato wa Mabadiliko mfumo wa uendeshaji ambapo sasa wanasubiri kuitishwa kwa Mkutano Mkuu wa Wanachama mwezi ujao
Uongozi wa Yanga haukutumia njia za mkato kwani wameshirikisha Serikali katika kila hatua ili kuhakikisha Mabadiliko wanayofanya yanakwenda sambamba na matakwa ya sheria za nchi
Watani zao Simba wametakiwa kuanza upya mchakato wao baada kukiuka taratibu za kisheria
Miezi michache iliyopita Tume ya Ushindani (FCC) ilitangaza kufanya uchunguzi wa mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Simba baada ya kubaini kuwepo kwa sintofahamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Mohammed Dewji jana alithibitisha kuwa FCC wamewaagiza waanze upya mchakato wao wa Mabadiliko
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said amesema Yanga haitaki kufanya makosa ndio maana imeishirikisha Serikali katika kila hatua
Tayari uongozi wa Yanga umetoa tamko la kuwataka Wanachama wake walipie ada zao za mwaka kuelekea kuitishwa kwa Mkutano Mkuu mwezi ujao
Mkutano huo wa mwaka huenda ukatumika kupitisha Mapendekezo ya mfumo uliopendekezwa na La Liga kisha ukaridhiwa na kamati ya Mabadiliko ya Yanga