Kikosi cha Yanga kujifua Gym mara tatu kwa wiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Dec 2017
Kikosi cha Yanga kujifua Gym mara tatu kwa wiki
Katika jitihada za kuhakikisha wachezaji wake wanakuwa fiti muda wote, kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ameongeza mazoezi ambapo sasa watakuwa wakifanya mazoezi ya Gym mara tatu kwa wiki.

Lwandamina amedhamiria kuiona Yanga inatetea ubingwa wake wa VPL kwa msimu wa nne huku msimu huu akiipa kipaumbele michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Amesema kwa ratiba ya michuano ya klabu bingwa ilivyo, haoni sababu kwa Yanga kutotinga hatua ya makundi.

Aidha kurejea kwa Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko kumemuongezea matumaini kocha huyo asiye na maneno mengi.

Amesema Yanga itaboreka zaidi baada ya wachezaji hao wote kurejea.

Wakati Tambwe akiwa amerejea kwa asilimia 100, Ngoma na Kamusoko tayari wameanza mazoezi mepesi.

Ngoma anatarajiwa kurejea dimbani mwezi Januari 2018 kukiwa na uwezekano wa kutumika kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi.

Kamusoko huenda akahitaji hadi wiki tatu kuwa tayari kurejea dimbani kulingana na daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’