Jana viongozi wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla walifika Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao ambacho Serikali iliagiza kifanyike baina yao na TFF kumaliza sintofahamu inayojitokeza baina ya pande hizo
Wiki iliyopita Serikali iliagiza pande mbili kukutana na kumaliza tofauti zao kisha kuwasilisha uamuzi wao kama mrejesho baada ya Yanga kulalamika Wizarani kuonewa na TFF
Kikao hicho kilianza saa nne asubuhi na kumalizika majira ya mchana


Hakuna kiongozi wa Yanga wala TFF aliyekuwa tayari kubainisha kilichozungumzwa lakini ajenda kuu ilikuwa malalamiko ya klabu ya Yanga kutotendewa haki na TFF katika masuala mbalimbali
Kufungiwa kwa Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela kulipelekea uongozi wa Yanga kuwasilisha malalamiko yao Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Serikali kuagiza pande hizo kukutana na kupata mwafaka