Baadhi ya wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo walipewa mikataba ya miezi sita ambayo inawezwa kuhuishwa kama viwango vyao vitawaridhisha mabosi wa kamati ya usajili Yanga
Mshambuliaji Fiston Abdul Razak ni miongoni mwa wachezaji hao ambao wana mikataba ya muda mfupi
Nyota huyo aliyetua Yanga akitokea kule Misri, ameanza kwa kusua sua mpaka sasa akiwa ametupia bao moja
Ni mshambuliaji ambaye wengi walikuwa na matumaini makubwa kuwa ataongeza makali ya safu ya ushambuliaji ambayo pia inaundwa na kina Michael Sarpong, Ditram Nchimbi, Yacouba Songne na Waziri Junior
Hata hivyo Fiston bado ana takribani mechi 10 za kuwashawishi Wanayanga ili kuona kama mkataba wake unaweza kuhuishwa mwezi Juni
Aidha Farid Mussa ni mchezaji mwengine ambaye mkataba wake utamalizika mwezi Juni
Farid alitua Yanga akitokea Hispania, awali akisaini mkataba wa mwaka mmoja