Mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa wataendelea kupambana kuhakikisha wanatimiza lengo la kushinda ubingwa msimu huu
Metacha hakuwa sehemu ya kikosi kilicholazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi kuu uliopita dhidi ya KMC
Mlinda lango huyo mwenye cleansheet 11 msimu huu, amesema wamepania kuirejesha furaha ya mashabiki wao, ni suala la muda tu
"Furaha itarejea na amani itakuwepo na msimu huu tutakuwa bingwa kwa hali yoyote wakati utaongea Inshaallah," Metacha ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Yanga inaendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Biashara United ambao utapigwa Jumamosi, April 17 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE