Match Day : Yanga vs KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2021
Match Day : Yanga vs KMC

Baada ya mapumziko ya mwezi mzima kupisha kalenda ya michuano ya Kimataifa pamoja na maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, awamu ya tano Hayati Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga leo wanarejea 'mzigoni' pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku

Wananchi watakuwa pale kwa Mkapa kuwakabili KMC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 24

Hii ni ngwe ya lala salama, ni mchezo ambao Yanga inahitaji alama zote tatu ili kuendelea kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema wamejiandaa vizuri kukabiliana na KMC leo kwa kucheza soka la burudani na sio kukaa nyuma kuhakikisha wanapata ushindi

Amesema kikosi chake kitaingia uwanjani wakiwa na tahadhari kubwa wakijua wanakutana na timu nzuri na ngumu

Nae nahodha wa Yanga Lamine Moro, amesema wapo tayari kupambana kwani anajua ni mchezo mgumu na katika kipindi chote alichokuwa Yanga hajawahi kukutana na mechi nyepesi, hivyo ni jukumu lao wachezaji kuipigania timu

Moro aliongeza kuwa bado hawajakata tamaa ya kuwania ubingwa akiwaalika mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono

Yanga leo itawakosa wachezaji wanne ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali

Yassin Mustafa na Farid Mussa ni wagonjwa wakati Haruna Niyonzima anakosekana kwa kuwa alichelewa kurejea kambini akitokea Rwanda kwenye majukumu ya Kimataifa

Kiungo Carlinhos anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, leo akimalizia adhabu hiyo aliyopewa katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ken Gold mwezi uliopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’