Dhamira ya ubingwa iko palepale - Mwambusi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2021
Dhamira ya ubingwa iko palepale - Mwambusi

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amesema dhamira ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu haijabadilika

Yanga imekaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa takribani miezi sita lakini bado wapo watu wanaamini Wananchi hawatakuwa na ubavu wa kutwaa ubingwa mbele ya watani zao Simba ambao wako nyuma kwa tofauti ya alama nne na michezo mitatu ya viporo

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari Makao Makuu ya klabu ya Yanga mapema leo, Mwambusi amesema dhamira ya kutwaa ubingwa iko palepale

"Dhamira yetu ya kutwaa ubingwa iko palepale. Nadhani hakuna mtu ambaye anaweza kusema Yanga haiko katika mpango wa kuwania ubingwa kwani mpaka sasa iko kileleni mwa msimamo wa ligi na timu nyingine zinafuatia," alisema Mwambusi

Aidha kuhusu maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya KMC utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Mwambusi amesema wamejiandaa vya kutosha, amefanyia kazi baadhi ya changamoto zilizokuwepo awali na mashabiki watarajie kuona mabadiliko kuanzia mchezo huo

"Mpira ni sayansi kubwa sana, unaweza ukawa unalaumu mchezaji pasipo kujua sababu ni nini, makosa mengi yaliyokuwa yanafanyika mimi kama mwalimu ndiyo kazi yangu kuyarekebisha, tutarajie kuwa yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’