Ntibazonkiza aahidi ushindi mechi ya KMC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2021
Ntibazonkiza aahidi ushindi mechi ya KMC

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza amesema wamejiandaa kuwapa furaha mashabiki wao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC hapo kesho

Ntibazonkiza amerejea kikosini akiwa imara baada ya kupona majeraha ya nyonga yaliyomuweka nje kwa takribani miezi miwili

Nyota huyo aliyewahi kutamba barani Ulaya, amewataka mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi kwani wamejipanga kupambana katika kila mechi ili kujiimarisha kwenye uongozi wa ligi na kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa

"Namshukuru Mungu, nimerejea nikiwa fiti, ninaamini nitakuwa na kipindi kingine kizuri, mengine yataonekana kwa vitendo uwanjani, kikubwa ni kuwa na afya njema"

"Mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono, tumedhamiria kufanya vizuri katika michezo iliyobaki, tutapambana kwenye kila mchezo, watafurahi" alisema Ntibazonkiza

Kurejea kwa Ntibanzonkiza kumeongeza mzuka kwenye kikosi cha kocha Juma Mwambusi ambaye kesho ataiongoza Yanga katika mchezo wake wa kwanza akikaimu nafasi ya Kocha Mkuu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’