Ni mbinu tu ya kuinyamazisha Yanga 'kibabe'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Apr 2021
Ni mbinu tu ya kuinyamazisha Yanga 'kibabe'

Ni hivi Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela kwa makosa ambayo sio ya kwake binafsi

Yanga ilimtuma Mwakalebela kuzungumza na Wanahabari na kubainisha yote yaliyozungumzwa kwenye mkutano ule

Kama ni adhabu ilipaswa kupewa klabu ya Yanga na sio Mwakalebela kwani yeye alikuwa Mjumbe tu, na Mjumbe huwa 'hauwawi'

Lakini inashangaza kuona Kamati ya Maadili ya TFF imemshughulikia 'mjumbe' na kumuacha mwajiri wake ambaye ndiye aliyewakilishwa

Kupitia taarifa waliyotoa kwa Wanahabari jana, uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa Mwakalebela aliwasilisha kile alichotumwa na klabu hiyo kwa maana kama kuna makosa basi yawe ya Yanga

Uongozi wa Yanga unaamini adhabu hiyo imetolewa kama vitisho na kujaribu kuwafunga mdomo wasilalamikie yanayofanywa dhidi yao

Huu umekuwa utamaduni wa TFF, kuwashughulikia 'wale' wanaolikosoa Shirikisho hilo

Mwaka juzi ilitungwa kanuni ya mavazi na ikatumika dhidi ya aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa TFF

Kanuni hiyo ilitumika kwake tu na haijawahi kutumika tena tangu yeye alipoondolewa Yanga

Mambo haya ya kuwafungia watu yamefanyika sana wakati wa utawala wa Rais wa sasa wa TFF Wallace Karia pengine kuliko wakati mwingine wowote

Kwa hakika hapa kuna jambo haliko sawa katika uongozi wa Karia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’