Jana jioni Yanga walicheza mchezo w akirafiki dhidi ya African Lyon kule Kigamboni na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 3-0
Baada ya kukinoa kikosi chake kwa takribani wiki tatu, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi alihitaji mchezo huo ili kuangalia kwa kiasi gani wachezaji wake wameiva
Kwa hakika yako matumaini kuwa Wananchi wajiandae kwa Yanga mpya iliyosukwa kivingine na kocha Mwambusi
Ari, kasi na shauku ya ushindi ndio mambo yanayoonekana katika nyuso za wachezaji wa Yanga
Jambo moja kubwa ambalo wachezaji wanafikiria ni kuwapa furaha mashabiki kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu
Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, kama watachanga karata zao vizuri katika michezo iliyobaki, nafasi ya kutwaa ubingwa wanayo
Mtihani wa kwanza wa kocha Mwambusi ni Jumamosi hii pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC