TFF wajitathmini kwa kumfungia Mwakalebela

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2021
TFF wajitathmini kwa kumfungia Mwakalebela

Haya ni maoni binafsi ya aliyewahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick kufuatia kufungiwa kwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Ndugu Fredrick Mwakalebela.

Klabu ya Yanga ilisajiliwa tarehe 12/02/1935 na kujipatia hadhi ya taasisi. Ikiwa kama taasisi, tarehe 19/02/2021 Klabu ya Yanga iliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa malalamiko yao jinsi gani kama taasisi inaona haitendewi haki ya shirikisho letu pendwa na tukufu.

Kwa mujibu wa katiba ya Yanga, Mwenyekiti, M/Mwenyekiti na Katibu Mkuu ndio watu pekee wana mamlaka ya kuongea kwa niaba ya taasisi hiyo. Kwaiyo Yanga kupitia M/Mwenyekiti wake aliongea kwa niaba ya Klabu na sio mambo yake binafsi.

Ibara ya 18(a) &(c) ya Katiba ya JMT inawapa haki watanzania wote na taasisi za kitanzania haki ya kujieleza, hivyo alichokifanya Mwakalebela kwa niaba ya Yanga ni kwa mujibu ya Katiba ya JMT, hivyo sheria yoyote inayokinzana na katiba ya nchi, hiyo sheria ni batiri.

Yanga sio Klabu ya kwanza kulalamika kwenye vyombo vya habari, wapo viongozi wengi wamekua wakilalamika kwenye vyombo vya habari, mfano ni yale maneno ya Kiongozi flani ya tarehe 1/11/2020 kupitia ukurasa wake wa Instagram alilalamika Klabu yake kufanyiwa dhulma, na kwenda mbali kusema mpira wetu wa Tanzania kamwe hauwezi kusonga mbele, kauli hii kwangu haina tofauti na msimamo ya Yanga kupitia M/Mwenyekiti.

Kwa style hii ni ngumu kuinua soka la Tanzania, CHAN tumeshatolewa, tukiachana na hamasa tunapaswa kama Taifa kuwa na mkakati maalumu wa kuinua mpira wetu.

Viongozi wote wa nchi hii wa sasa na waliopita wanaiheshimu hii taasisi, hivyo niwaombe wadau wote wa mpira Tanzania kuiheshimu Klabu ya Yanga ata kama hauishabikii kwani Kulwa na Dotto hutegemeana kwa namna moja au nyingine.

Mh. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo akiapisha makatibu wakuu kasema michezo ni ajira, ametoa rai kwa viongozi wote wa serikali kusapoti taasisi za michezo na kutatua kero zao kwani zinabeba mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Sihitaji kushauri nini cha kufanya, ila ni muda muafaka wa kutumia fursa hii kusaidia maendeleo ya mpira wetu.

Tanzania ni yetu sote na mpira wa Tanzania ni wetu sote.

Simon Patrick, Lawyer

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’