Mara paap! mwamba karejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2021
Mara paap! mwamba karejea

Ukipita kwenye kurasa za mitandao ya kijamii utakutana na tetesi nyingi zinazomuhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusufu Manji ambaye anatajwa kuwa mbioni kurejea nchini

Ukitaja jina la Manji kuna watu wanatetemeka kwani wanakumbuka kipindi ambacho alikuwa Mwenyekiti wa Yanga, hakuna timu iliyothubutu kutamba ndani ya ardhi ya Tanzania mbele ya Yanga

Changamoto alizopata mwishoni mwa mwaka 2016 zilipelekea ajiuzulu nafasi yake na kujikita katika kushughulikia kesi zilizokuwa zikimkabili

Na hata baada ya kufanikiwa kushinda kesi zote, Manji alilazimika kusafiri nje ya nchi kwenda kutibiwa maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua

Gazeti moja la michezo limedai kuwa Manji yuko mbioni kurejea nchini kuendelea na maisha yake

Wananchi wanatamani kuona pale atakaporejea, aingie kwenye uwekezaji Yanga

Yanga iko katika mchakato wa kubadili mfumo wake wa uendeshaji ambapo mchakato huo utakapokamilika, utatoa nafasi kwa wawekezaji kununua hisa asilimia 49 zitakazowekwa sokoni

Kulingana na mwongozo wa Serikali, hisa hizo zinapaswa kumilikiwa na wawekezaji watatu au zaidi

Manji anaweza kuwa na nafasi ya kununua hisa kuwa miongoni mwa wawekezaji

Wakati GSM wakitarajiwa kuwa Wawekezaji namba moja, pia yuko Rostam Aziz ambaye kampuni yake ya Taifa Gas inaidhamini Yanga

Wafanyabiashara hawa watatu wanaweza kuifanya Yanga ikawa timu ya kipekee barani Afrika kama itatokea wote wakawa wanahisa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’