Kocha Mkuu wa timu ya AS Vita Florente Ibenge amekiri kuwa kikosi chake kimepoteza makali baada ya kuwapoteza wachezaji wake muhimu waliosajiliwa na timu nyingine
Juzi AS Vita ilifungwa mabao 4-1 na Simba katika mchezo wa ligi ya mabingwa, kipigo hicho kiliwaondosha katika michuano hiyo
Ibenge alisema timu yake imepoteza wachezaji wake wazuri ambao baadhi wako hapa Tanzania wakiitumikia klabu ya Yanga
"Kwa sasa timu za Tanzania zina pesa ndio maana utaona wachezaji wetu wazuri wanaondoka Congo kuja kucheza Tanzania, " Ibenge aliwaambia waandishi wa habari
Winga Tuisila Kisinda na kiungo Mukoko Tonombe walisajiliwa na Yanga, GSM wakitumia 'fedhwa' kuwan'goa nyota hao AS Vita
Kisinda na Mukoko walikuwa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Ibenge
Kwa msimu wa tatu mfululizo AS Vita wameshindwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa
Yanga iliboresha kikosi chake msimu huu wakilenga kushinda ubingwa ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao