Sisi ndio wababe wao, tukutane May 08

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Apr 2021
Sisi ndio wababe wao, tukutane May 08

Ndivyo wananchi wanavyosema baada ya 'kuwacheki' watani zao Simba wakipata mafanikio kwenye michuano ya ligi ya mabingwa wakifanikiwa  kutinga robo fainali

Simba imepata matokeo mazuri katika michuano hiyo, Wananchi wanasema tambo zao wazifanyie hukohuko hapa nyumbani mfalme ni mmoja tu, Yanga

Upo msemo wa binti mdogo ambaye kipande cha video aliyorekodi imetamba sana kwenye mitandao ya kijamii akiwashangaa mashabiki wa Simba wanaoitambia Yanga baada ya kupata mafanikio huko nje

"Unawafunga wengine unaitambia Yanga, kunguru sio njiwa...!"

Timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa duru ya kwanza VPL, matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1

Simba walilazimika kusubiri mpaka dakika ya 87 kusawazisha bao kupata sare ambayo waliishangilia kwelikweli

Zilipokutana kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kule visiwani Zanzibar, ni Yanga iliyoibuka kidedea kwa ushindi wa mikwaju ya penati baada ya suluhu ya bila kufungana

Katika mchezo ule, Yanga walikuwa bora zaidi, pengine walistahili kushinda ndani ya dakika 90

Yanga bado wanaendelea kuwa wafalme wa 'dabi' pamoja na kuwa misimu mitatu iliyopita wamepita katika msukosuko mkubwa wa kiuchumi

Katika misimu miwili Simba imepata ushindi mara moja tu mbele ya Yanga katika michuano ya kombe la FA

Kwenye ligi huu ni msimu wa pili Simba haijafanikiwa kuondoka na ushindi mbele ya Yanga

Msimu uliopita walipata sare mchezo wa kwanza na wakafungwa katika mchezo wa pili

Msimu huu mechi ya kwanza ilimalizika kwa sare na mechi ya pili itapigwa May 08

Wananchi wana kila sababu ya kutamba, kwani ndio wababe wao...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’