Yanga kutoa tamko kifungo cha Mwakalebela

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2021
Yanga kutoa tamko kifungo cha Mwakalebela

Keshokutwa Jumanne uongozi wa klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla unatarajiwa kutoa tamko baada ya kufungiwa kwa Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela

Juzi Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilitangaza kumfungia Mwakalebela kifungo cha miaka mitano baada ya kumpata na hatia ya makosa mawili, uchochezi na kutoa taarifa ya uongo

Mwakalebela pia alipigwa faini ya jumla ya Tsh Milioni saba kutokana na makosa hayo ambayo kulingana na taarifa ya kamati ya Maadili, imeeleza aliyafanya katika mikutano aliyofanya na Wanahabari Oktoba 1 2020 na Februari 19 2021

Miongoni mwa hatua za haraka ambazo zinatarajiwa kuchukuliwa na Yanga ni kukata rufaa kupinga kifungo hicho cha Mwakalebela

Ni hivi karibuni Yanga ilishinda rufaa ya kifungo dhidi ya Mkuu wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano Hassan Bumbuli aliyekuwa amefungiwa miaka mitatu na Kamati hiyo hiyo ya Maadili kwa makosa ya kutoa taarifa za uongo

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’