Baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza alitarajiwa kuingia kambini leo kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa Jumamosi ijayo
Kulingana na Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli, Ntibazonkiza na Niyonzima walitarajiwa kuwasili leo kuuunga na wenzao
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa kwa mara ya kwanza wanaweza wakamshuhudia Ntibazonkiza akiitumika katika mchezo unaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Tangu asajiliwe kwenye usajili wa dirisha dogo, Ntibazonkiza ameitumikia Yanga katika mechi tatu za mikoani pamoja na kombe la Mapinduzi kule visiwani Zanzibar
Bila shaka mwamba huyu ataongeza nguvu kwenye mchezo dhidi ya KMC
Sasa yuko fiti kwa asilimia 100 baada ya kucheza mechi zote mbili za timu ya Taifa ya Burundi dhidi ya Afrika ya Kati na Morocco akifunga bao moja