Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe amesema atashirikiana na wachezaji wenzake kuhakikisha wanapambania kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu
Mukoko amerejea kutoka DR Congo ambako alikwenda kuitumikia timu yake ya Taifa katika mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 dhidi ya Gabon na Gambia
"Nimerejea kupambana ili kuhakikisha tunafikia malengo ya kushinda ubingwa. Hili ndilo kusudio letu ingawa nafahamu katika mzunguuko wa pili ushindani utakuwa mkubwa"
"Kama hatutafanikiwa itakuwa bahati mbaya sana, wakati mwingine mpira una matokeo ya kikatili lakini sisi wachezaji hakuna tunachofikiri zaidi ya kushinda ubingwa"
Mukoko ni miongoni mwa wachezaji watatu wa kigeni waliokuwa wameitwa kwa ajili ya majukumu ya timu zao za Taifa
Wengine ni Saido Ntibazonkiza (Burundi) na Haruna Niyonzima (Rwanda)