April 10, Yanga inaendelea na kampeni ya kusaka ubingwa wa 28 ligi kuu ya Vodacom kwa kuwakaribisha KMC katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku
Hesabu za Wananchi ni kuhakikisha wanakusanya alama tatu katika kila mchezo ili kufikia malengo ya kuibuka mabingwa
Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Kaimu Kocha Mkuu Juma Mwambusi ambaye alirejeshwa kuchukua mikoba iliyoachwa na Cedric Kaze aliyetimuliwa mwezi uliopita baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha
Timu hizi zilikutana jijini Mwanza mchezo wa duru ya kwanza ambao Waziri Junior aliihakikishia Yanga ushindi muhimu akifunga bao la pili katika ushindi wa mabao 2-1
KMC wamekuwa na kawaida ya 'kuivimbia' Yanga timu hizo zinapokutana lakini Wananchi hawako tayari kuona wanakosa alama zote tatu katika mchezo ujao
Kocha Mwambusi ameaminiwa kuivusha Yanga mpaka mwishoni mwa msimu, hatakuwa tayari kuona timu yake inashindwa kupata matokeo katika mchezo wake wa kwanza