Rwanda na Burundi zimeshindwa kufuzu fainali za Afcon baada ya kushindwa kupata matokeo muhimu katika michezo yao ya mwisho iliyopigwa jana usiku
Kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza na kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi waliikabili Morocco katika mchezo ambao Burundi walikubali kipigo cha bao 1-0
Aidha, Niyonzima aliiongoza Rwanda katika mchezo dhidi ya Cameroon, mchezo uliomalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Burundi imemaliza katika nafasi ya tatu kundi E nyuma ya Morroco na Mautitania zilizofuzu wakati Rwanda imemaliza nafasi ya tatu kundi F nyuma ya Cameroon na Cape Verde zilizofuzu
Saido na Haruna sasa wanarejea kuendelea na majukumu yao ndani ya klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE