Yanga inasubiri kutangaza Mzabuni aliyeshinda Tenda ya ujenzi wa uwanja wake kule Kigamboni
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema Makampuni yasiyopungua 10 kutoka ndani na nje ya nchi, wamejitosa kuwania tenda hiyo
Mfikirwa amesema wakati wowote watamtangaza mshindi wa tenda hiyo aweze kuanza ujenzi
Kuanzia msimu ujao, Yanga imepania kutumia viwanja vyake kwa ajili ya mazoezi Mzabuni akitakiwa kuanza kutengeneza uwanja vya nyasi asili na bandia
Wakati huohuo Yanga inaendelea na maboresho ya jengo lake lililoko Makao Makuu Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam
Baada ya zoezi la kupiga rangi, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wameendelea kujitolea kukarabati vyumba
Jengo hilo litatumika kwa ajili ya kambi za timu ya vijana na Wanawake
Aidha uwanja wa Kaunda nao uko katika mpango huo wa ukarabati