Kiungo wa Yanga Mukoko Tomombe jana aliitumikia timu yake ya Taifa ya DR Congo kwa dakika zote 90 katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 dhidi ya Gambia
Katika mchezo huo, DR Congo ilichomoza na ushindi wa bao 1-0

Mukoko alicheza kwa takribani dakika 30 katika mchezo uliopita dhidi ya Gabon, mchezo ambao DR Congo walifungwa mabao 3-0 na kupoteza matumaini ya kufuzu Afcon 2021
Aidha baada ya mchezo, Mukoko alipata nafasi ya kuonana na kocha wa viungo wa timu ya Taifa ya Gambia Riedoh Berdien ambaye msimu uliopita na mwanzoni mwa msimu huu alikuwa akiitumikia klabu ya Yanga

Kwa sasa yuko Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini
ADVERTISE HERE