Licha ya kuondoshwa katika kinyan'ganyiro cha kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Afcon 2021, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imemaliza mchezo wake wa mwisho kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Libya
Bao pekee la Stars liliwekwa kambani na winga Saimon Msuva aliyemalizia kwa kichwa krosi murua kutoka kwa Deus Kaseke ambaye leo alipata nafasi ya kuanza
Ni matokeo ambao hayabadili chochote katika msimamo wa kundi J kwani Tanzania imemaliza nafasi ya tatu ikiwa na alama saba
Tunisia na Guinea ya Ikweta tayari zimejihakikishia tiketi ya kushiriki michuano hiyo





ADVERTISE HERE