Baada ya kuvunja benchi la ufundi lililokuwa chini ya Kocha Cedric Kaze, Yanga inaendelea kuliunda upya benchi lake baada ya kumuongeza kocha wa magolikipa Razak Siwa
Siwa alikuwa akiinoa klabu ya Bandari Fc ya Kenya. Hii sio mara yake ya kwanza kutua Yanga, amewahi kufanya kazi na Wananchi miaka ya nyuma
Siwa ndiye aliyewapika makipa kama Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na bila ya kumsahau Farouk Shikhalo aliyekuwa nae Bandari Fc
Ameletwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Vladimir Niyonkuru
ADVERTISE HERE