Kocha Mpya ataongeza ari kikosini - Senzo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2021
Kocha Mpya ataongeza ari kikosini - Senzo

Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa amesema wameamua kumleta kocha mpya mapema kwa lengo la kuongeza nguvu katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu pamoja na michuano ya kombe la FA

Yanga iko katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kumpata kocha mpya ikielezwa mtaalamu huyo atatua nchini wakati wowote

Senzo amesema baada ya kufanya tathmini, pamoja na kumuamini kocha Juma Mwambusi, wanaamini ujio wa kocha mpya utawaongezea wachezaji ari mpya

"Tumeona ni lazima tupate kocha mpya haraka na mchakato ulikuwa unaendelea na sasa tupo katika hatua ya mwisho kabisa, tunataka kuhakikisha kabla ya timu haijarejea uwanjani tuwe tayari ameshakuja," Senzo alinukuliwa na Mwanaspoti

“Tunaona kuna nafasi kubwa ya kuwa bingwa msimu huu bila kujali tulivyoteleza hapa kati, huu ni upepo tu na umepita hatua muhimu ni kuinuka na kuendelea na safari kwa umakini"

"Siyo hatumuamini Mwambusi, tunaheshimu kazi kubwa anayofanya sasa na hata kabla kocha Mwambusi lakini tunataka kumuongezea mtu ambaye atasaidiana naye kuweza kufikia malengo yetu"

"Hata kocha atakayekuja tutataka afanye kazi na Mwambusi ili aweze kumsaidia kujua historia ya kikosi na hata aina ya ligi ya hapa hataweza kufanikiwa bila kuwa na msaada wa aina ya Mwambusi," aliongeza Senzo

Wakati Wananchi wakisubiri kutambulishwa kwa kocha huyo, kikosi kinaendelea na mazoezi Avic Town, Kigamboni kujiandaa na mechi za kuhitimisha msimu

Ligi itarejea baada ya kumalizika siku 21 za maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Tano, hayati Dk John Magufuli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’