Leo ni siku nyingine ngumu kwa Watanzania ambao tuko katika maombolezo ya kumpoteza aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Tano, Hayati Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 kutokana na maradhi ya moyo
Hii Leo mwili wa Hayati Magufuli utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya familia mjini Chato
Misa ya mazishi itafanyika katika uwanja wa Magufuli baada ya mwili kutoka kanisani kwa ibada maalumu
Rais Magufuli atazikwa na maelfu ya Watanzania ambao wamekuwa katika huzuni kubwa tangu kifo chake kilipotangazwa Machi 17
Wengi wamesafiri Chato kushiriki mazishi yake, lakini wengine watashuhudia maziko hayo 'mbashara' katika runinga
ADVERTISE HERE