Tanzania haitashiriki fainali za Afcon 2021 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Guinea ya Ikweta
Guinea ya Ikweta na Tunisia zimefuzu kwa michuano hiyo baada ya matokeo ya mechi za leo
Tunisia imeichapa Libya mabao 5-2 imefuzu ikiwa vinara wa kundi J ikiwa na alama 13
Tanzania haikuwa na mchezo mzuri leo, kocha Kim Poulsen akitumia mbinu za kujihami zaidi
Jitihada za kusaka alama moja zilikwamishwa kwenye dakika ya 88 Guinea ya Ikweta walipopata bao lao la ushindi
Tanzania haikuwa na madhara kabisa kwenye lango la Guinea ya Ikweta wakishindwa kupiga hata shuti moja lililolenga lango
Kama sio uhodari wa mlinda lango Aishi Manula pengine Tanzania ingefungwa mabao mengi
March 29 watakamilisha ratiba kwa mchezo dhidi ya Libya ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Tanzania na Libya zote zimetupwa nje ya michuano hiyo