Jana kiungo Haruna Niyonzima akiwa nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda, aliwaongoza 'Amavubi' kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Msumbiji na kufufua matumaini ya kufuzu fainali za Afcon 2021 zitakazofanyika nchini Cameroon mwishoni mwa mwaka huu
Kina Metacha Mnata, Yassin Mustafa, Bakatri Nondo, Feisal Salum, Farid Mussa na Deus Kaseke ni sehemu ya kikosi cha Tanzania killichosafiri Guinea ya Ikweta kwa ajili ya mchezo muhimu wa kuwania kufuzu Afcon kwa mara ya pili mfululizo

Mcongomani Mukoko Tomombe naye atakuwa na timu ya Taifa ya DR Congo ambayo baadae leo itacheza na Gabon


Mwamba Saido Ntibazonkiza ambaye amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu, kesho atakiongoza kikosi cha Burundi katika mchezo dhidi ya Afrika ya Kati
ADVERTISE HERE