Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo saa nne usiku kwa saa za Tanzania, itashuka Estadio de Malabo kuikabili Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fanali za Afcon 2021
Huu ni mchezo muhimu kwa Tanzania inayosaka nafasi ya kucheza Afcon kwa mara ya pili mfululizo
Ni mchezo ambao Tanzania inahitaji ushindi au matokeo ya sare kuelekea mchezo wao wa mwisho dhidi ya Libya ambao utapigwa jijini Dar es salaam Machi 29
Guinea ya Ikweta inashika nafasi ya pili kundi J ikiwa na alama sita wakati Tanzania iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne
Kama Guinea ya Ikweta watashinda leo basi watajihajihakikishia kufuzu Afcon 2021 wakiungana na Tunisia
Lakini matokeo tofauti yanaweza kuipa nafasi Tanzania kutegemeana na matokeo ya mechi za mwisho Tanzania ikicheza na Libya wakati Tunisia watacheza na Guinea ya Ikweta
Jana jioni vijana wa kocha Kim Poulsen walifanya maandalizi yao ya mwisho Estadio de Malabo kuelekea mchezo huo
Kila la kheri Stars