Morocco atamba mafanikio ya Zanzibar Heroes

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
18 Dec 2017
Morocco atamba mafanikio ya Zanzibar Heroes
Licha ya kupoteza mchezo wa fainali ya kombe la Chalenji, kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Ali ‘Morocco amesema, anajivunia mafanikio aliyoyapata ikiwa ni kuifikisha fainali timu yake ingawa hakufanikiwa kutwa taji hilo.

“Mimi ni kocha mdogo kuliko makocha wote, nimeweza kuifikisha timu fainali najivunia sana kwa mafanikio tuliyopata ukilinganisha na timu nyingine zilivyojiandaa na timu yetu ilivyokuwa underdogs imeweza kufika fainali si kitu cha kubeza.”

Morocco amewashukuru watanzania wote kwa ujumla kutokana na kuiunga mkono Zanzibar tangu hatua ya makundi hadi fainali.

“Tunawashukuru watanzania wote kwa kipindi chote ambacho tulikuwa kwenye mashindano haya kwa kutupa support na kututia moyo, nafikiri tumeweza kuonesha kwamba tunaweza kupambana kwa hiyo maisha yanaendelea baada ya fainali hii tutajipanga ili kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi katika mashindano mengine.”

Bingwa wa mashindano hayo (Kenya) wamezawadiwa kombe, medali pamoja na dola za Marekani 30,000 wakati washindi wa pili (Zanzibar Heroes) wakipatiwa medali na dola 20,000 huku washindi wa tatu (Uganda) wakipewa medali na dola 10,000.

Shaffih Dauda
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →