Mkufunzi wa Yanga Princess, Edna Lema 'Mourinho' amesema kuwa bado wana matumaini ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake, licha ya tofauti ya pointi moja dhidi ya watani zao Simba Queens ambao wanaongoza ligi
Yanga Princess walipoteza uongozi wa ligi baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba Queens, katika mchezo uliopita.
Simba Queens wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 39 wakati Yanga Princess wanashika nafasi ya pili wakijikusanyia alama 38
Lema amesema tofauti ya alama moja ni ndogo sana, wataendelea kupambana kuhakikisha wanashinda michezo yote iliyobaki
"Kikosi changu kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri msimu huu, na ikiwezekana kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake licha ya kwamba tuko nyuma kwa pointi moja dhidi ya viongozi wa ligi.
"Pointi moja kwenye soka ni ndogo sana, na lolote linaweza kutokea hivyo kila mtu acheze na kushinda mechi zake, kuhusu bingwa tutamjua mwishoni," amesema
Kwa sasa ligi kuu ya Wanawake umesimama kwa zilivyo ligi nyingine zote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya nne hayati Dk John Magufuli
Serikali ilitangaza siku 21 za kuomboleza msiba huo wa kitaifa uliotokea Machi 17