Msafara wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' unaondoka leo nchini Kenya kuelekea Guinea ya Ikweta kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021
Tanzania iliyokuwa imeweka kambi Kenya, keshokutwa Alhamisi itashuka dimbani ugenini huko Guinea ya Ikweta kusaka matokeo muhimu ambayo yatabainisha hatma ya Tanzania katika michuano hiyo
Tanzania inashika nafasi ya tatu kundi J ikiwa na alama nne nyuma ya Guinea ya Ikweta yenye alama sita
Hivyo Stars haipaswi kufungwa mchezo huo, matokeo yanayohitajika zaidi ni ushindi
Kocha Kim Poulsen ameondoka na msafara wa wachezaji 30

ADVERTISE HERE