Kocha Mpya wa Yanga anaweza kuwasili mapema kuungana na Juma Mwambusi imefahamika
Uongozi wa Yanga bado haujaweka hadharani jina la kocha huyo. Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla alitangaza kuwa Mwambusi anaweza kukiongoza kikosi michezo 11 iliyobaki kumaliza msimu
Hata hiyo imeonekana, upo umuhimu wa kocha mpya kuwasili mapema angalau kupata nafasi ya kukiona kikosi (uwanjani) ili afanye maamuzi sahihi katika maboresho yanayotarajiwa kufanywa mwishoni mwa msimu
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Dominic Albinus amesema mchakato wa kusaka kocha mpya unaendelea
"Tunaendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya, wakati huu timu itaendelea kuwa chini ya Mwambusi. Kocha mpya atakapopatikana, atakuwa na muda wa kuifahamu timu kwanza kabla ya kuanza majukumu yake akisaidiana na Mwambusi," alisema Albinus
Yanga iliachana na kocha Cedric Kaze baada ya mfululizo wa matokeo mabaya tangu kuanza kwa duru la pili ligi kuu ya Vodacom
Kwa sasa Mwambusi ameachiwa majukumu yote akiaminiwa katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu pamoja na michuano ya kombe la FA