Kweli Tambwe amerejea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2017
Kweli Tambwe amerejea
Amissi Tambwe jana aliitumikia Yanga kwa mara ya kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi ikiwa ni miezi minne imepita tangu aonekane dimbani August 20.

Tambwe jana alicheza dakika zote 90 za mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Vijana wa Polisi Tanzania wanaoshiriki ligi daraja la kwanza walitoa upinzani mkali kwa Yanga, na kitendo cha Tambwe kuweza kumaliza dakika zote tisini ni ishara njema kuwa mkali huyo wa mabao amerejea sasa.

Katika kikosi kilichoanza jana, Tambwe aliongoza safu ya ushambuliaji akisaidiana na Yusuph Mhilu/Geofrey Mwashiuya na Emanuel Martin/Yahana Mkomola.

Washambuliaji tegemeo Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa walipumzishwa kwenye mchezo huo.

Kwa kuwa amekaa nje muda mrefu bado atahitaji kucheza mechi zaidi ili aweze kurejesha makali yake ya kupachika mabao.

KIKOSI KILICHOCHEZA JANA
Beno Kakolanya/Youthe Rostand dk46, Juma Abdul, Hassan Kessy/Burhan Akilimali dk46, Nadir Haroub 'Cannavaro', Andrew Vincent 'Dante', Pato Ngonyani/Said Juma 'Makapu' dk50, Pius Buswita, Maka Edward/Papy Kabamba Tshishimbi dk46, Amissi Tambwe, Yussuf Mhilu/Geoffrey Mwashiuya dk46 na Emmanuel Martin/Yohanna Nkomola dk74.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’