Bosi Kaizer Chiefs aitabiria Yanga makubwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2021
Bosi Kaizer Chiefs aitabiria Yanga makubwa

Mkurugenzi Mkuu wa tathmini, Usajili na Maendeleo klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Walter Steenbok ameeleza kuvutiwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na klabu ya Yanga akiamini watafanikiwa katika mipango yao

Jana Steenbok aliwaongoza wenzake kutoka nchi za Afrika Kusini, Latvia na Uganda kuonana na Viongozi, Wafadhili, Wadhamini na Wahisani wa Klabu ya YangaΒ  kujadili maswala mbalimbali kuhusu soka la Bara la Afrika na uwekezaji endelevu kwenye vipaji vya soka hususani katika klabu ya Yanga

Wadau hao pia walitembelea Makao Makuu ya klabu ya Yanga na kujionea mambo mbalimbali

Steenbok ameeleza kushangazwa na ukubwa wa Yanga, kwa uwekezaji wanaofanya, wana nafasi ya kuwa kitovu cha soka Tanzania

"Yanga ni timu kubwa sana, nimeona wao ni klabu ya michezo mbalimbali, wana mashabiki wengi. Nimeona miundombinu yao, wana nafasi kubwa ya kuwa kitovu cha soka hapa Tanzania. Nimevutiwa na duka lao ambalo wanauza jezi na bidhaa nyingine za klabu, nimeshuhudia watu wengi wakifika kununua jezi. Ni chanzo kizuri cha mapato"

"Ni jambo zuri kuwa na mipango, kuweka malengo na kuhakikisha unafikia malengo yako. Jambo muhimu pia wanapaswa kuwa na mfumo mzuri wa kukuza wachezaji kuanzia umri mdogo miaka 9,11 na kuendelea. Huu ndio utaratibu ambao timu kubwa zinafanya," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’