Mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom pamoja na kombe la FA itarejea mwanzoni mwa mwezi April baada ya siku 14 za kusimamishwa michezo kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, marehemu Dk John Magufuli
Vinara wa ligi hiyo Yanga wao wataanza na mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kule mkoani Rukwa, uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga April 02/03
Baada ya mchezo huo, Wananchi watarejea jijini Dar es salaam ambapo watacheza michezo minne dhidi ya KMC, Biashara United, Gwambina Fc na Azam Fc
April 24 Wananchi watakuwa mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Namungo Fc
Hii hapa Ratiba ya mwezi April

ADVERTISE HERE