Nahodha Msaidizi wa Yanga Mukoko Tomombe ameondoka nchini jana kuelekea DR Congo kujiunga na timu ya Taifa
Mukoko ni mmoja wa wachezaji watatu wa kigeni ndani ya kikosi cha Yanga ambao wameitwa timu za Taifa

Wengine ni Saido Ntibazonkiza (Burundi) na Haruna Niyonzima (Rwanda)
Aidha, wachezaji wengine nane wameitwa timu ya Taifa ya Tanzania. Nyota hao ni Metacha Mnata, Yassin Mustafa, Dickson Job, Bakari Nondo Mwamnyeto, Feisal Salum, Deus Kaseke, Farid Mussa na Ditram Nchimbi
Mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon zinatamatishwa mwishoni mwa mwezi huu Tanzania ikitarajiwa kusafiri Guinea ya Ikweta kwa ajili ya mchezo ambao utapigwa March 24 kisha kurejea jijini Dar es salaam kuhitimisha michuano hiyo kwa kuikabili Libya March 29
ADVERTISE HERE