Zanzibar Heroes yafa kiume Kenya, yachapwa kwa matuta

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2017
Zanzibar Heroes yafa kiume Kenya, yachapwa kwa matuta
Harambee Stars imefanikiwa kutwaa taji la CECAFA Senior Challenge baada ya kuifunga Zanzibar kwa mikwaju 3-2 ya penati kufuatia sare ya mabao 2-2 baada ya dakika 120.

Kenya imetwaa taji hilo kwa mara ya saba.

Ochieng Ovella alianza kuifungia Kenya bao la mapema kwenye dakika ya 05 kupitia mpira wa adhabu.

Kenya ilitawala zaidi kwenye kipindi cha kwanza lakini hivyo Zanzibar Heroes ilirejea mchezoni kwenye kipindi cha pili na ilifanikiwa kusawazisha bao dakika tatu kabla dakika 90 za mchezo kukamilika mfungaji akiwa Khamis Mussa Makame aliyeunganisha vyema krosi ya Haji Mwinyi Mngwali aliyewatoka walinzi wa Kenya kabla ya kumimina majaro ya chinichini kwa mfungaji.

Bao hilo lilipelekea mchezo huo kuongezwa dakika 30 za nyongeza baada ya kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Ni Kenya tena iliyotangulia kufunga bao la pili kwenye dakika ya 98 mfungaji akiwa na Masoud Juma lakini Khamis Mussa Makame akaisawazishia Zanzibar dakika mbili baadae.

Licha ya mashambulizi ya hapa na pale baada ya kuingia kwa mabao hayo, mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 baada ya dakika 120 kukamilika.

bahati haikuwa upende wa Zanzibar kwani katika changamoto ya mikwaju ya penati, mlinda lango wa Kenya alifanikiwa kudaka mikwaju mitatu ya Zanzibar na kuisaidia timu yake iibuke na ushindi wa mikwaju 3-2.

Vijana wa Zanzibar Heroes wanastahili pongezi za dhati licha ya kukikosa kikombe hicho ilichokitwaa kwa mara ya mwisho dhidi ya Kenya mwaka 1995 tena kupitia mikwaju ya penati

Ari, morali na kujituma kwa wachezaji wa Zanzibar Heroes kumewawesha kutinga fainali ya michuano hiyo licha ya kutopewa nafasi kwenye hatua za mwanzo.

Bila shaka ndugu zao wa Kilimajaro Stars walioambulia alama moja pekee na kuaga mapema wana cha kujifunza kupitia mafanikio iliyopata Zanzibar Heroes.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’