Mwambusi abadili program ya mazoezi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Mar 2021
Mwambusi abadili program ya mazoezi Yanga

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Juma Mwambusi amebadili program ya mazoezi ya vijana wake kuhakikisha wanakuwa sawa kabla ya kurejea kwa mikiki mikiki ya ligi kuu na kombe la FA mwezi ujao

Mwambusi aliyekabidhiwa mikoba iliyoachwa na Cedric Kaze amewasilisha program ya mazoezi ambayo siku ya Jumatatu mpaka Alhamisi wachezaji watafanya program tofauti na siku ya Ijumaa

Katika program hiyo,  siku Nne za mwanzo vijana watafanya mazoezi mara mbili kisha Ijumaa watafanya mara moja.

Mwambusi amesema anaamini vijana wake watakuwa sawa huku akiangalia uwezekano wa kupata mchezo wa kirafiki kabla ya ligi kurejea

"Programu hii imelenga kurejesha utimamu wa mwili kwa wachezaji lakini pia kujenga uwezo wa pamoja kama timu kutokana na mapungufu ambayo yalionekana kwenye kikosi," alisema

Mtihani wake wa kwanza utakuwa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Sumbawanga, April 04

Mwambusi ni kocha mwenye uzoefu mkubwa na michezo ya aina hii hivyo bila shaka ataweza kuivusha Yanga salama kuelekea robo fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’