FT : Yanga 0-0 Polisi Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2017
FT : Yanga 0-0 Polisi Tanzania
Yanga SC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Polisi Tanzania katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wachache, Yanga ilishindwa kabisa kutegua mitego ya Polisi ili kupata bao.

Pamoja na benchi la ufundi la Yanga kubadili karibu wachezaji wote kipindi cha pili, akiwaingiza nyota wa kikosi cha kwanza akina Youthe Rostande, Papy Kabamba Tshishimbi, Geoffrey Mwashiuya na Burhan Akilimali kuchukua nafasi za Benno Kakolanya, Hassan Kessy, Maka Edward na Yusuph Mhilu, lakini mambo yaliendelea kuwa magumu.

Kiungo Pius Buswita aliikosesha Yanga bao la wazi dakika ya 57 baada ya kushindwa kumalizia krosi ya Geoffrey Mwashiuya.

Akicheza kwa mara ya kwanza msimu huu, mshambuliaji Mrundi Amissi Joselyn Tambwe aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu alikaribia kufunga dakika ya 64 kama si mpira alioupiga kwa kichwa kufuatia krosi ya Burhan Akilimali kwenda nje.

Polisi nao walikaribia kupata bao dakika ya 66 baada ya shuti la Ahmad Kambangwa kwenda nje sentimita chache.
Buswita tena dakika ya 76 akaunganishia nje kwa shuti dhaifu kona ya Juma Abdul kabla ya dakika ya 80 mchezaji wa zamani wa Mbao FC kumtilia pasi nzuri Akilimali aliyepiga shuti lililotua mikononi mwa kipa wa Polisi, Kondo Salum.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Beno Kakolanya/Youthe Rostand dk46, Juma Abdul, Hassan Kessy/Burhan Akilimali dk46, Nadir Haroub 'Cannavaro', Andrew Vincent 'Dante', Pato Ngonyani/Said Juma 'Makapu' dk50, Pius Buswita, Maka Edward/Papy Kabamba Tshishimbi dk46, Amissi Tambwe, Yussuf Mhilu/Geoffrey Mwashiuya dk46 na Emmanuel Martin/Yohanna Nkomola dk74.

Polisi Tanzania; Kondo Salum/Ally Abdul dk84, James Ambrose, Juma Ramadhan, Lakini Mwakalukwa, Ezekiel Lawi, Abdallah Mudhihiri, Benedicto Elius/Ahmad Kambangwa dk49, Jeremiah Katula, Jackson Wawa, Tizzo Chomba na Ally Mabuya.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’