Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Nyayo
Ulikuwa ni mchezo wa kujipima nguvu kuziandaa timu zote kwa ajili ya mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021
Erick Kapaito na Abdallah Hassan walifunga mabao ya Kenya wakati bao la Tanzania lilifungwa na Ayoub Lyanga
Timu hizo zitarudiana tena Alhamisi, March 18 katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Kasarani
Tanzania watakuwa wenyeji wa mchezo huo licha ya kuwa utapigwa hukohuko Kenya
ADVERTISE HERE