Kwa Ratiba hii ubingwa unawezekana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Mar 2021
Kwa Ratiba hii ubingwa unawezekana

Yanga ilianza duru ya pili na ratiba ngumu sana ambayo kwa hakika ilikuwa ni lazima wangeacha alama mahali

Ni bahati mbaya tu waliacha alama nyingi mpaka kupelekea benchi la ufundi kufutwa kazi

Walianza duru ya pili na mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, wakafuata Mbeya City, wakarudi Dar kuikabili Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kabla ya kuelekea mikoa ya Tanga na Arusha kucheza na Coastal Union na Polisi Tanzania

Kwa kuangalia ratiba ya mechi zilizobaki, ni wazi wananchi wavute pumzi kwani michezo mingi wataimalizia nyumbani ukilinganisha na watani zao Simba ambao nao itakuwa zamu yao 'ku-suffer'

Katika michezo 11 iliyobaki, Wananchi wana michezo saba ya nyumbani dhidi ya KMC, Biashara United, Gwambina Fc, Azam Fc, Ihefu Fc, Simba na Mwadui Fc

Wakati mechi zilizobaki ugenini ni dhidi ya Namungo Fc, Ruvu Shooting, Dodoma Jiji na JKT Tanzania

Mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utapigwa jijini Dar es salaam hivyo Yanga watasafiri mikoa miwili tu kwenda Lindi (vs Namungo) na Dodoma (vs Dodoma Jiji na JKT Tanzania) 

Kwa upande wa watani zao Simba michezo waliyobaki nayo nyumbani ni dhidi ya Dodoma Jiji, Coastal Union, Mtibwa Sugar, Yanga, Mbeya City na Namungo Fc

Wakati michezo ya ugenini ni dhidi ya Kagera Sugar, Namungo Fc, KMC, Polisi Tanzania, Gwambina Fc, Ruvu Shooting, Mwadui Fc na Azam Fc

Simba wana mechi sita nyumbani na mechi nane ugenini pamoja na kuwa baadhi ya mechi za ugenini watacheza Dar

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’